KUELEKEA TAMASHA LA "DODOMA MPYA CONCERT"... BASATA YAIPONGEZA KAMPUNI YA MILLENNIUM STARS ENTERTAINMENT, YAAHIDI USHIRIKIANO

Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) limeahidi kutoa ushirikiano katika Shughuri mbalimbali zinazoandaliwa na Kampuni ya Millennium Stars Entertainment zenye lengo la Kuinua na kukuza Sanaa nchini Tanzania. Hatua hiyo ya BASATA imekuja baada ya Kampuni ya Millennium Stars Entertainment kuitikia wito kutoka Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kujadili juu ya Tamasha la "DODOMA MPYA CONCERT" lenye dhamira ya kuhamasisha ujio wa makao makuu ya Serikali Mkoani Dodoma.
 Katika hatua nyingine Baraza la Sanaa la Taifa limeahidi kutoa ushirikano wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hilo la kihistoria nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa mtaalamu  atakayesaidia katika kutoa ushauri na maelekezo katika kufanikisha Tamasha hilo.

Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na  Matukio (BASATA) ndugu. Kurwijira Maregesi
Upande wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment uliwakilishwa na ndg. Amiri Kilizo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sanaa, Muziki na Utamaduni ndani ya Kampuni ya Millennium Stars Entertainment huku BASATA ikiwakilishwa na watendaji mbalimbali wa Baraza hili ikiwa ni pamoja  Katibu Mkuu wa Baraza hilo ndg. Godfrey Mngereza na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na  Matukio (BASATA) ndugu. Kurwijira Maregesi .  Ushirikiano uliopo kati ya Kampuni ya Millennium Stars Entertainment na BASATA unaonyesha kuwa na Tija kubwa kwa sanaa nchini Tanzania.


0 comments: