latest articles

SANAA IKIPEWA KIPAUMBELE INAWEZA KUAJIRI WATU WENGI KULIKO SEKTA YOYOTE

Kampuni ya Millennium Stars Entertainment imeendelea kutoa Elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikusanyiko isiyo rasmi, vikao na wadau mbali mbali na mitandao ya kijamii juu ya umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa sekta ya  sanaa na utamaduni kwani ina uwezo wa kuajiri watu wengi kama zilivyo Sekta nyingine. 
           Baadhi ya wasanii wakifanya mazoezi kuboresha kazi zao.
Read more

MKURUGENZI WA MILLENNIUM STARS ENTERTAINMENT ATEMBELEA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC)

Ikiwa ni muendeleo wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment kuendelea kutafuta fursa mbalimbali za kiuwekezaji na kujenga mahusiano na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ametembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania kanda ya kati Dodoma na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kituo cha uwekezaji (Tanzania Investment Center -TIC)  ndugu Martin Masalu.

Katika Mazungumzo kati ya Mkurugenzi wa Millennium Stars Entertainment ameupongeza uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa jinsi wanavyofanya kazi kubwa kuwaunganisha watanzania na wawekezaji toka maeneo mbalimbali Duniani lakini pia kwa kuzitangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
                      Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) akimuelekeza Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowasa kuhusiana na Shughuri mbalimbali za TIC. (Picha haihusiani na habari)
Read more

MH. MAVUNDE KUCHANGIA GHARAMA ZA USAJIRI WA VIKUNDI 10 VYA SANAA KUPITIA TAMASHA LA DODOMA MPYA

Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde ameahidi kulipia gharama za kusajiri Vikundi 10 chini ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA ikiwa ni sehemu ya kusaidia Kurasimisha kazi za Sanaa nchini. Mheshimiwa Mavunde ametoa ahadi hiyo akiwa Ofisini kwake Mkoani Dodoma baada ya Kutembelea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment ndg. Josias Charles ambaye alifika Ofisini kwa Mh. Mavunde kuzungumza nae juu ya Umuhimu wa Tamasha la Dodoma Mpya linalotarajia kufanyika kuanzia Tarehe 5/08/2017 na kuzunguka wilaya zote 7 za Dodoma huku hitimisho likifanyika katika uwanja wa Jamhuri Stadium kama taarifa zitakavyotolewa hapo baadae.


Mh. Antony Peter Mavunde, (Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na walemavu.
Read more

KUELEKEA TAMASHA LA "DODOMA MPYA CONCERT"... BASATA YAIPONGEZA KAMPUNI YA MILLENNIUM STARS ENTERTAINMENT, YAAHIDI USHIRIKIANO

Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) limeahidi kutoa ushirikiano katika Shughuri mbalimbali zinazoandaliwa na Kampuni ya Millennium Stars Entertainment zenye lengo la Kuinua na kukuza Sanaa nchini Tanzania. Hatua hiyo ya BASATA imekuja baada ya Kampuni ya Millennium Stars Entertainment kuitikia wito kutoka Baraza la Sanaa la Taifa BASATA kujadili juu ya Tamasha la "DODOMA MPYA CONCERT" lenye dhamira ya kuhamasisha ujio wa makao makuu ya Serikali Mkoani Dodoma.
 Katika hatua nyingine Baraza la Sanaa la Taifa limeahidi kutoa ushirikano wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hilo la kihistoria nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa mtaalamu  atakayesaidia katika kutoa ushauri na maelekezo katika kufanikisha Tamasha hilo.

Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na  Matukio (BASATA) ndugu. Kurwijira Maregesi
Read more

MAMBO 5 YA AJABU YALIYOWAHI KUPATIKANA UFUKWENI (BEACH)

Read more

Wahalifu Wanne Wauwawa Katika Mapambano Na Polisi Kibiti

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

Read more

MWIGULU AWATAHADHARISHA LEMA NA MNYIKA

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewatahadharisha Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema na Mbunge wa Kibamba Mh. John Mnyika kuwa makini na kauli zao juu ya suala la mauaji linaloendelea Kibiti Mkoani Pwani.

Mh. Mwigulu alitoa Kauli hiyo jana bungeni kufuatia kauli zilizotolewa na wabunge hao wakati mijadala mbalimbali ikiendele bungeni.
Kuendelea Kupata taarifa kama hizi endelea Kutembelea Millennium TV na ku follow mtandao wetu wa Tweeter/Millennium TV

Read more

TAKUKURU yafunguka Baada ya Kuwakamata Jamal Malinzi, Mwesigwa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania, (Takukuru) imethibitisha kumshikiria Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na katibu wake, Mwesigwa Silentine kwa mahojiano ambayo hakuyaweka wazi.

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Mussa Misalaba amethibisha kuwa viongozi hao walikamatwa kwa ajili ya uchunguzi ambapo amesema kuwa Jamal Malinzi na wengine wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali.

Kuhusu ufafanuzi wa tuhuma hizo, ofisa huyo alikataa kuzitaja kwamba ni suala la kiuchunguzi.

Pia alipoulizwa sasa ni lini viongozi hao watafikishwa mahakamani alisema hawezi kusema kwani inawezekana kama watuhumiwa hao wakitoa ushirikiano kwa Takukuru wa ushahidi wanaweza wasifikishwe mahakamani.


Credit : Udaku Special Blog.
Read more