MH. MAVUNDE KUCHANGIA GHARAMA ZA USAJIRI WA VIKUNDI 10 VYA SANAA KUPITIA TAMASHA LA DODOMA MPYA

Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde ameahidi kulipia gharama za kusajiri Vikundi 10 chini ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA ikiwa ni sehemu ya kusaidia Kurasimisha kazi za Sanaa nchini. Mheshimiwa Mavunde ametoa ahadi hiyo akiwa Ofisini kwake Mkoani Dodoma baada ya Kutembelea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment ndg. Josias Charles ambaye alifika Ofisini kwa Mh. Mavunde kuzungumza nae juu ya Umuhimu wa Tamasha la Dodoma Mpya linalotarajia kufanyika kuanzia Tarehe 5/08/2017 na kuzunguka wilaya zote 7 za Dodoma huku hitimisho likifanyika katika uwanja wa Jamhuri Stadium kama taarifa zitakavyotolewa hapo baadae.


Mh. Antony Peter Mavunde, (Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na walemavu.

Mheshimiwa Mavunde ambaye amevutiwa kwa kiwango Kikubwa na utendaji kazi wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment ameahidi kuendelea Kuipatia Ushirikiano wa kutosha Kampuni hiyo kwa kadri itakavyowezekana ili kukuza Sanaa na utamaduni Nchini Tanzania.
Tamasha la Dodoma Mpya Concert linatarajiwa kutumika Kuhamasisha Shughuri mbalimbali za Kiuchumi kuelekea Ujio wa Serikali Mkoani Dodoma kama Makao makuu huku likilenga Kuibua Vikundi Vipya vya sanaatakribani 10 kwa kila wilaya na kuhakikisha Vinasajiriwa na kutambulika chini ya Baraza la Sanaa la Taifa ikiwa ni namna ya kurasimisha kazi za Sanaa na utamaduni nchini.

Mpaka hitimisho la Tamasha hili litakapofanyika inakadiliwa kuwa litakua limeweza kuwafikia zaidi ya Vikundi 70 vipya vya sanaa sawa na zaidi ya wasanii 700. Mafanikio ya Tamasha hili itakua chachu kubwa kwa maendeleo ya Mkoa wa Dodoma lakini pia itakua mafanikio makubwa katika Tasnia ya Sanaa nchini.
Josias Charles (Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment Company Ltd





1 comment: