SANAA IKIPEWA KIPAUMBELE INAWEZA KUAJIRI WATU WENGI KULIKO SEKTA YOYOTE

Kampuni ya Millennium Stars Entertainment imeendelea kutoa Elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikusanyiko isiyo rasmi, vikao na wadau mbali mbali na mitandao ya kijamii juu ya umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa sekta ya  sanaa na utamaduni kwani ina uwezo wa kuajiri watu wengi kama zilivyo Sekta nyingine. 
           Baadhi ya wasanii wakifanya mazoezi kuboresha kazi zao.
Katika jitihada za kuendelea kuipigania Sanaa na Utamaduni kuwa miongoni mwa Sekta rasmi na zenye kuchangia pato kubwa kwa Taifa kama ilivyo kwa Nchi zilizoendelea kama Marekani na China kampuni ya Millennium Stars Entertainment imeendelea kuwahamasisha wananchi na viongozi mbali mbali  wa Sekta binafsi na Serikali kuendelea kuithamini na kuipa kipaumbele Sanaa kwani bado nchini Tanzania sanaa iko chini ukilinganisha na Nchi nyingine.


Katika Upande mwingine Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment ametoa wito kwa wasanii kuendelea kuheshimu kazi zao na kuzifanya kwa nidhamu na kwa weledi ili kuendelea kuleta taswira nzuri kwa jamii.
"Unajua kwa sasa watu wengi wanaichukulia sanaa kama kitu cha ziada na wanaifanya bila weledi hali inayofanya sanaa kuendelea kudharauliwa na jamii. Ninaamini kama wasanii wataitambua nguvu ya sanaa na wakaifanya kitaaluma naamini jamii itaanza kuona thamani ya Sanaa" Alisema Josias Charles

0 comments: