MKURUGENZI WA MILLENNIUM STARS ENTERTAINMENT ATEMBELEA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC)

Ikiwa ni muendeleo wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment kuendelea kutafuta fursa mbalimbali za kiuwekezaji na kujenga mahusiano na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ametembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania kanda ya kati Dodoma na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kituo cha uwekezaji (Tanzania Investment Center -TIC)  ndugu Martin Masalu.

Katika Mazungumzo kati ya Mkurugenzi wa Millennium Stars Entertainment ameupongeza uongozi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa jinsi wanavyofanya kazi kubwa kuwaunganisha watanzania na wawekezaji toka maeneo mbalimbali Duniani lakini pia kwa kuzitangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania.
                      Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) akimuelekeza Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Lowasa kuhusiana na Shughuri mbalimbali za TIC. (Picha haihusiani na habari)


Miongoni ma mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na namna ya kuzidi kupanua wigo katika suala zima la uwekezaji katika Sanaa nchini Tanzania. Mkuu huyo wa kituo cha Uwekezaji Tanzania ameahidi kuendelea kuwaunganisha wawekezaji mbalimbali na wadau wa sanaa ili kuzidi kukuza sekta hiyo yenye nafasi kubwa ya kutoa fursa za ajira Nchini.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Kituo cha Uwekezaji amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Kampuni ya Millennium Stars Entertainment  katika kupambana kurasimisha shughuri za Sanaa Nchini na kuhamasisha wadau kuthamini sanaa kama chachu ya maendeleo.

0 comments: